سَتَجِدُونَ ءَاخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأۡمَنُوكُمۡ وَيَأۡمَنُواْ قَوۡمَهُمۡ كُلَّ مَا رُدُّوٓاْ إِلَى ٱلۡفِتۡنَةِ أُرۡكِسُواْ فِيهَاۚ فَإِن لَّمۡ يَعۡتَزِلُوكُمۡ وَيُلۡقُوٓاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ وَيَكُفُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡۚ وَأُوْلَٰٓئِكُمۡ جَعَلۡنَا لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينٗا ٩١
Satajidūna ākharīna yurīdūna an ya'manūkum waya'manū qawmahum kulla mā ruddū ilal-fitnati urkisū fīhā fa il lam ya'tazilūkum wayulqū ilaykumus-salama wayakuffū aydiyahum fakhudhūhum waqtulūhum haythu thaqiftumūhum wa ulā'ikum ja'alnā lakum 'alayhim sultānam mubīnā
Mtawakuta wengine wanataka wapate salama kwenu na salama kwa watu wao. Kila wakirudishwa kwenye fitna hudidimizwa humo. Ikiwa hawajitengi nanyi, na wakakuleteeni salama, na wakazuia mikono yao, basi wakamateni na wauweni popote mnapo wakuta. Na juu ya hao ndio tumekupeni hoja zilizo wazi. 91
Maelezo ya chini
91 Mkiwashinda washirikina, hao wanaafiki huwa pamoja nanyi; na washirikina wakiwashinda Waislamu, wao huwa pamoja na washirikina. Wao hutaka wapate amani kwa Waislamu na wapate amani kwa jamaa zao washirikina. Hawa wamo katika upotovu na unaafiki wa moja kwa moja. Ikiwa hawatoacha kukupigeni vita na wakakutangazieni amani na salama, basi wauweni popote muwapatapo. Kwani kwa kuto kujitenga na kukupigeni vita, basi inakuwa Waumini wana haki kuwauwa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa Waumini hoja iliyo wazi kuwapiga vita.