وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطٗا ١٢٦
Walillāhi mā fis-samāwāti wamā fil-ardi wakānallāhu bikulli shay'im muhītā
Ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuvizunguka vitu vyote. 126
Maelezo ya chini
126 Hakika wa kumtakasia niya ni Mwenyezi Mungu, na ndio kwake Yeye inapasa uusilimishe uso wako, yaani umuelekee na umnyenyekee. Huko ndiko kumsafia niya Mwenyezi Mungu aliye umba ulimwengu wote, na ndiye mwenye kuumiliki. Vitu vyote viliomo mbinguni na duniani - nyota, sayari, jua, mwezi, milima, mabonde, majangwa, mashamba n.k. ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kubainikiwa na kila kitu, Mwenye kujua kwa ujuzi mkamilifu wa kuvizunguka vitu vyote avitendavyo mwanaadamu. Na Yeye atamlipa kheri akitenda kheri, na shari akitenda shari.