Surat An-Naml, aya 64

27:64

أَمَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَمَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٦٤

Amman yabda'ul-khalqa thumma yu'īduhū waman yarzuqukum minas-samā'i wal-ardi a'ilāhum ma'allāhi qul hātū burhānakum in kuntum sādiqīn

Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli. 64

Maelezo ya chini

64 Bali waulize, ewe Mtume: Nani anaye anzisha uumbaji tangu mwanzo, na kisha baada ya kupotea kwake akaurejesha kama ulivyo kuwa? Na nani anaye kuteremshieni riziki kutoka mbinguni, na akaitoa kwenye ardhi? Hakuna mungu pamoja na Mwenyezi Mungu atendaye hayo. Sema, ewe Mtume, kuwatahayarisha na kuwakanya: Kama nyinyi mnaye mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu basi tupeni hoja ya hayo, ikiwa mnadai kuwa nyinyi ni wasema kweli. Na wala hayataweza kuwa hayo kwenu.