Surat Al-Qasas, aya 27

28:27

قَالَ إِنِّيٓ أُرِيدُ أَنۡ أُنكِحَكَ إِحۡدَى ٱبۡنَتَيَّ هَٰتَيۡنِ عَلَىٰٓ أَن تَأۡجُرَنِي ثَمَٰنِيَ حِجَجٖۖ فَإِنۡ أَتۡمَمۡتَ عَشۡرٗا فَمِنۡ عِندِكَۖ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أَشُقَّ عَلَيۡكَۚ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ٢٧

Qāla innī urīdu an unkihaka ihdabnatayya hātayni 'alā an ta'juranī thamāniya hijajin fa in atmamta 'ashran famin 'indika wamā urīdu an ashuqqa 'alayka satajidunī in shā'allāhu minas-sālihīn

Akasema: Mimi nataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane. Ukitimiza kumi, khiari yako; lakini mimi sitaki kukutaabisha. Inshallah utanikuta miongoni mwa watu wema. 27

Maelezo ya chini

27 Shuaibu a.s. akamwambia: Mimi nataka kukuoza mmoja wa hawa mabinti zangu kwa mahari ya kunifanyia kazi muda wa miaka minane. Ukitimiza kumi itakuwa ni khiari yako. Wala mimi sitaki kukulazimisha huo muda mrefu. Na Inshallah, Mwenyezi Mungu akipenda, utaniona mimi ni katika watu wema, wenye kwenda nawe kwa ihsani na kutimiza ahadi.