Surat Al-Mulk, aya 21

67:21

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي يَرۡزُقُكُمۡ إِنۡ أَمۡسَكَ رِزۡقَهُۥۚ بَل لَّجُّواْ فِي عُتُوّٖ وَنُفُورٍ ٢١

Amman hādhal-ladhī yarzuqukum in amsaka rizqahū bal lajjū fī 'utuwwin wanufūr

Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na chuki. 21

Maelezo ya chini

21 Bali ni nani huyo atakaye kuruzukuni kwa yanayo kupeni uhai wenu na starehe zenu, ikiwa Mwenyezi Mungu akizuia riziki zake asikupeni? Bali makafiri wamekakamia katika kutakabari kwao na kuikimbia Haki.