إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ٱلۡأَذَلِّينَ ٢٠
Innal-ladhīna yuhāddūnallāha warasūlahū ulā'ika fil-adhallīn
Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho. 20
Maelezo ya chini
20 Hao wanao mfanyia inda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio katika hisabu ya walio fikilia ukomo wa udhalili.