وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦ فَأَعۡرَضَ عَنۡهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُۚ إِنَّا جَعَلۡنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ أَكِنَّةً أَن يَفۡقَهُوهُ وَفِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٗاۖ وَإِن تَدۡعُهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ فَلَن يَهۡتَدُوٓاْ إِذًا أَبَدٗا ٥٧
Waman azlamu mimman dhukkira bi'āyāti rabbihī fa a'rada 'anhā wanasiya mā qaddamat yadāhu innā ja'alnā 'alā qulūbihim akinnatan an yafqahūhu wafī ādhānihim waqran wa in tad'uhum ilal-hudā falan yahtadū idhan abadā
Na ni nani dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyo tangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uwongofu hawakubali kabisa kuongoka. 57
Maelezo ya chini
57 Na hapana yeyote aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko huyo anaye waidhiwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi naye asizingatie, na akasahau nini matokeo ya maasi yake anayo yatenda! Hakika Sisi kwa sababu ya kuelekea kwao kwenye ukafiri tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao, basi nyoyo zao hazitambui wala haziingii mwangaza. Na masikioni mwao tumetia uziwi basi hawasikii la kuwafahamisha! Nawe, ewe Mtume! Ukiwaita kwenye Dini ya Haki hawato ongoka maadamu tabia yao ni hii.