Surat Al-Isra, aya 28

17:28

وَإِمَّا تُعۡرِضَنَّ عَنۡهُمُ ٱبۡتِغَآءَ رَحۡمَةٖ مِّن رَّبِّكَ تَرۡجُوهَا فَقُل لَّهُمۡ قَوۡلٗا مَّيۡسُورٗا ٢٨

Wa immā tu'ridanna 'anhumubtighā'a rahmatim mir rabbika tarjūhā faqul lahum qawlam maysūrā

Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema nao maneno laini. 28

Maelezo ya chini

28 Ukilazimika kujikurupusha na hao walio tajwa wenye haja, kwa sababu ya shida uliyo nayo, na ukawa hukuwapa kwa kuto kuwa nacho cha kuwapa sasa, na ilhali unataraji Mwenyezi Mungu atakufungulia baadae, basi nena nao kwa maneno mema ya kuwapa imani nawe.