Surat Al-Isra, aya 2

17:2

وَءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَٰهُ هُدٗى لِّبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُواْ مِن دُونِي وَكِيلٗا ٢

Wa ātaynā mūsal-kitāba waja'alnāhu hudal libanī isrā'īla allā tattakhidhū min dūnī wakīlā

Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ila Mimi! 2

Maelezo ya chini

2 Na hakika hiyo Baitul Muqaddas ilikuwa inakaliwa na Wana wa Israili baada ya Musa, mpaka walipo fanya fisadi yao humo, wakafukuzwa hapo zamani. Haya ijapo kuwa Sisi tulimpa Musa Taurati, na tukatia ndani yake uwongofu, na tukawaambia: Msimfanye yeyote wa kumtegemezea mambo yenu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.