Surat Al-Imran, aya 41

3:41

قَالَ رَبِّ ٱجۡعَل لِّيٓ ءَايَةٗۖ قَالَ ءَايَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ ٱلنَّاسَ ثَلَٰثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمۡزٗاۗ وَٱذۡكُر رَّبَّكَ كَثِيرٗا وَسَبِّحۡ بِٱلۡعَشِيِّ وَٱلۡإِبۡكَٰرِ ٤١

Qāla rabbij'al lī āyatan qāla āyatuka allā tukalliman-nāsa thalāthata ayyāmin illā ramzan wadhkur rabbaka kathīran wasabbih bil-'ashiyyi wal-ibkār

Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama. Akasema: Alama yako ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipo kuwa kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Mola Mlezi wako kwa wingi na mtakase jioni na asubuhi. 41

Maelezo ya chini

41 Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi amfanyie alama ya kuhakikisha bishara hii. Mwenyezi Mungu akamjibu: Alama yako ni kuwa hutaweza kusema na watu muda wa siku tatu, isipo kuwa utatumia ishara tu kuashiria utakacho. Na shikamana na dhikri ya Mwenyezi Mungu ukimtakasa na kumtukuza jioni na asubuhi.