قُلۡ إِن كُنتُمۡ تُحِبُّونَ ٱللَّهَ فَٱتَّبِعُونِي يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٣١
Qul in kuntum tuhibbūnallāha fattabi'ūnī yuhbibkumullāhu wayaghfir lakum dhunūbakum wallāhu ghafūrur rahīm
Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. 31
Maelezo ya chini
31 Sema: Ikiwa nyinyi ni wakweli katika madai yenu, kuwa mnampenda Mwenyezi Mungu na mnataka Mwenyezi Mungu akupendeni, basi nifuateni mimi kwa ninayo kuamrisheni na ninayo kukatazeni. Kwani mimi nimetumwa na Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu atakupendeni kwa hivyo, na atakulipeni kwa kukufanyieni hisani na kusamehe makosa yenu. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kuwasamehe na kuwarehemu waja wake.