Surat Al-Imran, aya 21

3:21

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَيَقۡتُلُونَ ٱلَّذِينَ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡقِسۡطِ مِنَ ٱلنَّاسِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ٢١

Innal-ladhīna yakfurūna bi'āyātillāhi wayaqtulūnan-nabiyyina bighayri haqqin wayaqtulūnal-ladhīna ya'murūna bil-qisti minan-nāsi fabasshirhum bi'adhābin alīm

Hakika wanao zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali. 21

Maelezo ya chini

21 Hakika wale wanao zipinga Ishara za Mwenyezi Mungu katika uumbaji na hizi zilizo teremka, na wakawauwa Manabii alio watuma Mwenyezi Mungu waje kuwaongoa - bila ya haki kabisa, na hiyo ni dhulma kubwa mno - na wakawauwa wale wanao waita watu wafanye haki na uadilifu, watu hao wanastahiki adhabu kali. Basi wabashirie adhabu hiyo!