Surat Al-Imran, aya 11

3:11

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ١١

Kada'bi āli fir'awna walladhīna min qablihim kaddhabū bi'āyātinā fa akhadhahumullāhu bidhunūbihim wallāhu shadīdul-'iqāb

Kama yaliyo wapata watu wa Firauni na wale walio kuwa kabla yao. Walikanusha Ishara zetu, basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa madhambi yao; na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 11

Maelezo ya chini

11 Na hali ya hao ni kama hali ya kaumu ya Firauni walio kuwa na inda kabla yao. Walizikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu juu ya kuwa zilikuwa ziwazi kabisa. Basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa sababu ya madhambi waliyo yatenda. Na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.