Surat Al-Hijr, aya 86

15:86

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ ٨٦

Inna rabbaka huwal-khallāqul-'alīm

Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi. 86

Maelezo ya chini

86 Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu aliye kuumba na akakulea, ni Mwenye viumbe vyote, na anajua hali yako na yao. Yeye anastahiki umtegemezee mambo yako na yao. Naye anajua maslaha yako na yao.