فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ ٢٩
Fa idhā sawwaytuhū wanafakhtu fīhi mir rūhī faqa'ū lahū sājidīn
Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia. 29
Maelezo ya chini
29 Nikisha kamilisha kumuumba, na nikampulizia roho ambayo ninaimiliki, basi teremkeni kwa nyuso zenu mkimsujudia, kwa kumwamkia na kumhishimu.