Surat Al-Hashr, aya 19

59:19

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ نَسُواْ ٱللَّهَ فَأَنسَىٰهُمۡ أَنفُسَهُمۡۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ١٩

Walā takūnū kalladhīna nasullāha fa ansāhum anfusahum ulā'ika humul-fāsiqūn

Wala msiwe kama wale walio msahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio wapotovu. 19

Maelezo ya chini

19 Enyi Waumini! Msiwe kama wale walio sahau haki za Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao, kwa kuwajaribu kwa mitihani, na wakawa hawajui linalo wafaa na linalo wadhuru. Hao ndio walio toka wakaacha ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.