يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱرۡكَعُواْ وَٱسۡجُدُواْۤ وَٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمۡ وَٱفۡعَلُواْ ٱلۡخَيۡرَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ۩ ٧٧
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanurka'ū wasjudū wa'budū rabbakum waf'alul-khayra la'allakum tuflihūn
Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe. 77
Maelezo ya chini
77 Enyi mlio amini! Msishughulikie upotovu wa makafiri. Nyinyi endeleeni na kutimiza Swala zenu kwa ukamilifu kwa kurukuu na kusujudu. Na muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni na akakuruzukuni. Wala msimshirikishe naye na yeyote. Na tendeni kila lenye kheri na manufaa, ili mpate kuwa watu wema, walio bahatika katika Akhera yenu na dunia yenu.