Surat Al-Hajj, aya 10

22:10

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتۡ يَدَاكَ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيۡسَ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ ١٠

Dhālika bimā qaddamat yadāka wa annallāha laysa bizallāmil lil-'abīd

(Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya iliyo tanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhaalimu kwa waja. 10

Maelezo ya chini

10 Na ataambiwa: Hayo unayo yapata ya hizaya na adhabu ni kwa sababu ya uzushi wako na kiburi chako; kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Muadilifu, hadhulumu. Wala hawaweki sawa Muumini na kafiri, na mwema na muovu; bali kila mmoja wao atamlipa kwa mujibu wa vitendo vyake.