Surat Al-Baqarah, aya 84

2:84

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ لَا تَسۡفِكُونَ دِمَآءَكُمۡ وَلَا تُخۡرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ ثُمَّ أَقۡرَرۡتُمۡ وَأَنتُمۡ تَشۡهَدُونَ ٨٤

Wa idh akhadhnā mīthāqakum lā tasfikūna dimā'akum walā tukhrijūna anfusakum min diyārikum thumma aqrartum wa antum tashhadūn

Na tulipo chukua agano lenu kuwa hamtamwaga damu zenu, wala hamtatoana majumbani mwenu; nanyi mkakubali nanyi mnashuhudia. 84

Maelezo ya chini

84 Na kumbukeni tulipo chukua ahadi kwenu katika Taurat kuwa hamtakuwa mkimwaga damu zenu, wala hamtafukuzana katika majumba yenu. Na ahadi hiyo mnakubali kuwa ipo katika Kitabu chenu na mnashuhudia kuwa ni kweli.