فَإِن زَلَلۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡكُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ٢٠٩
Fa in zalaltum mim ba'di mā jā'atkumul-bayyinātu fa'lamū annallāha 'azīzun hakīm
Na ikiwa mkateleza baada ya kukufikieni hoja zilizo wazi, basi jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 209
Maelezo ya chini
209 Mkigeuka mkaiacha Njia hii mliyo itiwa muifuate nyote baada ya kudhihiri hoja za kukata kuwa ndiyo Njia ya Haki, basi jueni mtapatilizwa kwa kugeuka huko, kwani Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye nguvu, humuadhibu mwenye kuiacha Njia yake, na Mwenye hikima anaye pima kadiri ya adhabu yake.