Surat Al-Baqarah, aya 204

2:204

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ ٢٠٤

Waminan-nāsi man yu'jibuka qawluhū fil-hayawātid-dunyā wayushhidullāha 'alā mā fī qalbihī wahuwa aladdul-khisām

Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu. 204

Maelezo ya chini

204 Ilivyo kuwa kumcha Mwenyezi Mungu ndio msingi, basi khasara ni ya wale watu ambao dhamiri walio nayo nyoyoni mwao ni mbali na maneno yanayo tamkwa na ndimi zao. Wamepewa utamu wa kupanga maneno, hukufurahisha kauli yao katika kujivutia manufaa ya maisha ya kidunia, na kuunga mkono kwa wayasemayo humsingizia Mwenyezi Mungu kuwa anashuhudia kuwa wayasemayo yanatoka nyoyoni mwao. Kumbe wao kwa hakika ndio wakubwa wa ukhasama na ukhabithi kwako wewe.