Surat Al-A'raf, aya 98

7:98

أَوَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا ضُحٗى وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ ٩٨

Awa'amina ahlul-qurā an ya'tiyahum ba sunā duhan wahum yal'abūn

Au watu wa mijini wameaminisha ya kuwa adhabu yetu haitawafika mchana, nao wanacheza? 98

Maelezo ya chini

98 Je, watu hawa wameghafilika na wamejiaminisha kuwa adhabu haitawajia mchana kweupe na jua linawaka, nao wameshughulikia mambo yasiyo na faida nao?