وَكَم مِّن قَرۡيَةٍ أَهۡلَكۡنَٰهَا فَجَآءَهَا بَأۡسُنَا بَيَٰتًا أَوۡ هُمۡ قَآئِلُونَ ٤
Wakam min qaryatin ahlaknāhā fajā'ahā ba sunā bayātan aw hum qā'ilūn
Na miji mingapi tuliiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipo kuwa wamelala adhuhuri. 4
Maelezo ya chini
4 Kwani Sisi tumekwisha iteketeza miji kadhaa wa kadhaa, kwa sababu watu wao walikuwa wakiwaabudu wasio kuwa Mwenyezi Mungu, na kwa kuwa katika mwendo wao hawakufuata Njia yake. Ikawajia adhabu yetu wakati wao wameghafilika na wametuwa usiku nao wamelala, kama yalivyo wapata kaumu ya Lut'; au wakatekezwa mchana nao wamepumzika wakati wa kujinyoosha, kama yalivyo wapata kaumu ya Shua'ib.