فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ يَنَالُهُمۡ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوۡنَهُمۡ قَالُوٓاْ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ ٣٧
Faman azlamu mimmaniftarā 'alallāhi kadhiban aw kaddhaba bi'āyātihī ulā'ika yanāluhum nasībuhum minal-kitābi hattā idhā jā'athum rusulunā yatawaffawnahum qālū ayna mā kuntum tad'ūna min dūnillāhi qālū dallū 'annā washahidū 'alā anfusihim annahum kānū kāfirīn
Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au anaye zikanusha Ishara zake? Hao itawafikia sehemu yao waliyo andikiwa, mpaka watakapo wafikia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi mlio kuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea! Na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri. 37
Maelezo ya chini
37 Hapana wakubwa wa dhulma kuliko hao wanao mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa kumnasibisha na mshirika na mwana, na kuzua kuhalalisha na kuharimisha na mengineyo, pasina hoja. Au wanao kanusha Aya, Ishara, za Mwenyezi Mungu zilizo funuliwa katika Vitabu vyake na zinazo onekana katika ulimwengu wake. Hao wanapata hapa duniani sehemu ya aliyo waandikia Mwenyezi Mungu katika riziki, au uhai, au adhabu. Mpaka akiwajia Malaika wa Mauti kuzipokea roho zao, hapo huwaambia kwa kuwasuta: Iko wapi hiyo miungu yenu mliyo kuwa mkiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu ije kukukingeni na mauti? Nao wajibu: Wametukataa, wametuacha na wametukimbia. Na wajishuhudie wenyewe wakikiri kuwa hakika walikuwa makafiri.