وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُواْ مِنۡهُم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ ٤١
Walaqadistuhzi'a birusulim min qablika fahāqa billadhīna sakhirū minhum mā kānū bihī yastahzi'ūn
Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale walio wafanyia maskhara yaliwafika yale waliyo kuwa wakiyafanyia dhihaka. 41
Maelezo ya chini
41 Na Mitume wa kabla yako yaliwapata vile vile ya kufanyiwa kejeli na makafiri katika kaumu zao. Ikawateremkia hao walio wakataa Mitume na kuwafanyia maskhara adhabu hiyo hiyo ambayo wao waliifanyia maskhara na kejeli.