Surat Al-Anbiya, aya 34

21:34

وَمَا جَعَلۡنَا لِبَشَرٖ مِّن قَبۡلِكَ ٱلۡخُلۡدَۖ أَفَإِيْن مِّتَّ فَهُمُ ٱلۡخَٰلِدُونَ ٣٤

Wamā ja'alnā libasharim min qablikal-khulda afa'im mitta fahumul-khālidūn

Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele. Basi je! Ukifa wewe, wao wataishi milele? 34

Maelezo ya chini

34 Ewe Nabii! Hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako wewe aishi milele, hata ikawa hao makafiri wakawa wanakutamania ufe wewe. Vipi wanakutamania mauti wewe na hali na wao vile vile watakufa kama wewe? Ukifa wewe, je, ndio wao watabakia kushinda wanaadamu wote?