وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمۡ يُوحَ إِلَيۡهِ شَيۡءٞ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثۡلَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّٰلِمُونَ فِي غَمَرَٰتِ ٱلۡمَوۡتِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ بَاسِطُوٓاْ أَيۡدِيهِمۡ أَخۡرِجُوٓاْ أَنفُسَكُمُۖ ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَوۡنَ عَذَابَ ٱلۡهُونِ بِمَا كُنتُمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَكُنتُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِهِۦ تَسۡتَكۡبِرُونَ ٩٣
Waman azlamu mimmaniftarā 'alallāhi kadhiban aw qāla ūhiya ilayya walam yūha ilayhi shay'un waman qāla sa'unzilu mithla mā anzalallāhu walaw tarā idhiz-zālimūna fī ghamarātil-mawti wal-malā'ikatu bāsitū aydīhim akhrijū anfusakumul-yawma tujzawna 'adhābal-hūni bimā kuntum taqūlūna 'alallāhi ghayral-haqqi wakuntum 'an āyātihī tastakbirūn
Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake. 93
Maelezo ya chini
93 Nabii huyu hakusema uwongo alipo tangaza kuwa Qur'ani imetoka kwaMwenyezi Mungu. Na hapana mwenye kumshinda kwa udhaalimu huyo aliye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au akasema: Nimepata wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwa kapata wahyi wowote ule. Vile vile hapana dhaalimu mkubwa zaidi kuliko anaye sema: Mimi nitaleta maneno sawa na hayo aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa unaijua hali ya hao madhaalimu nao wamo katika shida za mauti, na Malaika wanazing'oa roho zao kutokana na miili yao, kwa ukali na nguvu, ungeli ona vitisho vya kushitua vinawashukia! Wakati huo hao huambiwa: Sasa malipo yenu ya adhabu ya kudhalilisha na kufedhehesha yanaanza. Malipo haya ni kwa vile mlivyo kuwa mkimzulia Mwenyezi Mungu bila ya haki, na ni malipo kwa kuwa kiburi chenu kilikuzuieni msiangalie na kuzipima Aya, Ishara, za uumbaji za Mwenyezi Mungu ziliomo katika Qur'ani.