Surat Al-An'am, aya 126

6:126

وَهَٰذَا صِرَٰطُ رَبِّكَ مُسۡتَقِيمٗاۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ ١٢٦

Wahādhā sirātu rabbika mustaqīman qad fassalnal-āyāti liqawmin yaddhakkarūn

Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi Iliyo nyooka. Tumezipambanua Aya kwa watu wanao kumbuka. 126

Maelezo ya chini

126 Na hii tuliyo ibainisha ndio Njia ya Haki Iliyo Nyooka. Nasi tumeipambanua na tumeiweka wazi kwa watu wote, na wala hawanufaiki kwayo ila wale ambao shani yao ni kukumbuka na kutaka hidaya.