Surat Al-An'am, aya 117

6:117

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِۦۖ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ ١١٧

Inna rabbaka huwa a'lamu man yadillu 'an sabīlihī wahuwa a'lamu bil-muhtadīn

Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio potea Njia yake, na ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio hidika. 117

Maelezo ya chini

117 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua kwa ujuzi ambao hapana mfano wake, kuwajua hao ambao wamekuwa mbali na Njia ya Haki, na hao ambao wameongoka na uwongofu ukawa ndio sifa yao.