وَٱتَّبِعۡ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا ٢
Wattabi' mā yūhā ilayka mir rabbika innallāha kāna bimā ta'malūna khabīrā
Na fuata uliyo funuliwa kwa wahyi kutokana na Mola wako Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda. 2
Maelezo ya chini
2 Na fuata wahyi unao teremka juu yako kutokana na Mola wako Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu anaye kufunulia kwa wahyi anazo khabari hata za mambo madogo madogo unayo yatenda wewe, na wanayo yatenda makafiri na wanaafiki.